Kitivo cha Utafiti wa Afrika cha Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang(IASZNU) ni kitivo cha kwanza cha utafiti wa kiujumla wa Afrika kilichoanzishwa na chuo kikuu nchini China. Kitivo hiki kiko mjini Jinhua, mkoa wa Zhejiang ulioko mashariki mwa China. Madhumuni ya kitivo hiki ni kujenga jukwaa la taaluma lililo wazi kwa upeo wa macho wa kimataifa wa kiwango cha juu, kukusanya watafiti hodari ndani na nje ya nchi, na kwa kupitia bidii ya miaka kadhaa, kujenga kitivo cha taaluma cha utafiti wa Afrika ambacho kina kozi za kila aina, kundi lenye watafiti hodari na usimamizi bora, ili kukidhi mahitaji ya mambo ya nje ya taifa, ujenzi wa kanda na maendeleo ya chuo kikuu.

Kitivo cha utafiti wa Afrika kina taasisi nne za utafiti : Taasisi ya Utafiti wa Siasa ya Afrika na Uhusiano wa Kimataifa, Taasisi ya Utafiti wa Uchumi wa Afrika, Taasisi ya Utafiti wa Elimu ya Afrika na Taasisi ya Utafiti wa Historia ya Afrika na utamaduni wake. Kinajitahidi kufanya utafiti wa kiujumla katika sekta kuu mbili yaani “masuala ya maendeleo ya Afrika katika enzi hii” na “ uhusiano kati ya China na Afrika katika enzi hii”. Aidha kinajaribu kufikia kiwango cha taaluma cha “upendo kwa Afrika, umaalum wa kichina na upeo wa macho wa dunia”.

Sasa wako wanataaluma ishirini na watatu katika kitivo. Miongoni mwao, kuna Profesa mmoja aliyepewa cheo maalum na serikali ya mkoa wa Zhejiang, Maprofesa wanne ( Maprofesa wawili wanaofundisha wanafunzi wa shahada ya juu), Maprofesa Wasaidizi watano, Wahadhiri kumi na sita( wote wamepata shahada ya juu) na Maprofesa wa Fahari na Watafiti Washiriki zaidi ya kumi. Kitivo hiki ni asasi kubwa kabisa inayoshughulikia utafitii wa Afrika miongoni mwa vyuo vikuu nchini China. Ujenzi wa kitivo hiki umefadhiliwa na Idara ya Afrika na Idara ya Mipango ya Wizara ya Mambo ya Nje, Kitivo cha Sayansi cha Jamii ya China, Chuo Kikuu cha Diplomasia, Taasisi ya Uhusiano wa Kimataifa ya China na Taasisi ya Mawasiliano ya Elimu ya Kimataifa ya China.

Kitivo kimemwalika Prof. Liu Hongwu ambaye ni mtaalamu maarufu wa utafiti wa Afrika nchini China kuja kufanya kazi kama Profesa maalum (yaani “Mwanachuo wa Qianjiang”) aliyepewa cheo na serikali ya mkoa wa Zhejiang na mkuu mtendaji wa kitivo, tena kimemwalika Prof. Gu Jianxin ambaye ni naibu mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje ya serikali ya mkoa wa Zhejiang kuja kufanya kazi kama naibu mkuu wa kitivo.

Kitivo kimetunga “Mkusanyiko wa Vitabu vya Utafiti wa Afrika wa Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang” na jarida ya kitivo “Utafiti wa Afrika”. Kimejenga Jumba la Makumbusho la Afrika, Kituo cha Uenezi wa Sanaa za Kiafrika na Kituo kinachoshughulikia maswali kuhusu biashara na uwekezaji barani Afrika. Kwenye Kituo cha Vitabu kuna vitabu zaidi ya 5000 vya sekta ya taaluma ya Afrika ( vitabu zaidi ya 1600 vya lugha za kigeni), zaidi ya aina 90 za majarida ( aina 34 za majarida ya lugha ya Kiingereza). Kitivo kimejenga tovuti (http://ias.zjnu.cn)ambapo Habari za Kitivo hutangazwa.

Katika Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang, kazi zinazoshughulikia mambo ya Afrika zilianza mnamo miaka ya 90 ya karne iliyopita ambapo taasisi ya mafundisho ya lugha ya Kichina ilianzishwa barani Afrika ( sasa kinaitwa Taasisi ya Confucius). Mwaka 2001, chuo kikuu kilianza kusimamia mradi wa mafunzo kwa Afrika kupitia Wizara ya Elimu na kikawa kituo cha msaada wa elimu kwa nje cha Jamhuri ya Watu wa China. Mwaka 2003, Taasisi ya Utafiti wa Elimu ya Afrika ilianzishwa. Mwaka 2006, semina ya kwanza ya wakuu wa vyuo vikuu vya China na Afrika ilifanyika. Mwaka 2007, Kitivo cha Utafiti wa Afrka kilianzishwa rasmi. Baada ya bidii ya zaidi ya miaka kumi, kazi zinazoshughulikia Afrika zimegusia kila pande na matokeo ya ujenzi wa jumla wa taaluma ya Afrika yameanza kutokea. Taasisi mbalimbali za utafiti zimeanzishwa kama vile Kituo cha Utafiti wa Sanaa ya Kiafrika, Taasisi ya Utafiti wa Jiografia ya Afrika, Taasisi ya Utafiti wa Mawasiliano ya Afrika, Kituo cha usambazaji wa lugha ya Kichina kwa Afrika, Taasisi ya Uchumi wa Afrika na Urusi n.k.

Kitivo cha Utafiti wa Afrika kimejenga uhusiano wa mawasiliano na ushirikiano wa kitaaluma na vyuo vikuu maarufu zaidi ya kumi vya Afrika. Kila mwaka walimu na wanafunzi wanaosomea shahada ya uzamili huchaguliwa na kwenda kufanya utafiti au kusomea vyuo vikuu vya Afrika. Mpaka sasa kozi mbili yaani Historia ya Afrika na Ulinganishi wa Elimu za Afrika zimeanza kuwatayarisha wanafunzi wa shahada ya pili na wanafunzi kutoka nchi za nje. Watafiti na wanafunzi wa shahada ya uzamili wamekwenda Tanzania na Kenya kufanya utafiti na kusoma kwa mara nyingi na hata mkuu wa kitivo Prof. Liu Hongwu ametunga kitabu maalum kinachoitwa “ Afrika Yenye Rangi ya Samawati----Utafiti wa Utamaduni wa Waswahili wa Afrika ya Mashariki”.

Kitivo kimepata matunda mengi ya utafiti ambayo umaalum wao ni wazi. Terehe 12, Novemba, mwaka 2008, kitivo kilifanya uzinduzi wa kitabu cha “Utafiti wa Suala la Darfur Kwa Upeo wa Macho wa Dunia” mjini Beijing ambacho ni kimojawapo katika vitabu vya kundi la kwanza vya “Mkusanyiko wa Vitabu vya Utafiti wa Afrika wa Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang”, tena kilifanya Semina ya Kimataifa ya Suala la Darfur. Katika mwaka mzima, kitivo kimepata maendeleo katika sekta ya siasa na uchumi wa Afrika, elimu ya Afrika, uhusiano kati ya China na Afrika n.k. na kimefuatiliwa na kutiwa maanani na pande mbalimbali.

Majengo ya makao makuu ya kitivo yenye mtindo wa kale yako kando ya Ziwa Xinyue, na jengo la Yifu na roshani ya Tonghui ni majengo makuu ya kitivo. Eneo la ofisi ni zaidi ya mita za mraba 2000. Humo ndani kuna zana za kisasa za kila aina, kituo cha mikutano, kumbi la hotuba ya taaluma, jengo la kuwapokea wataalamu, na ofisi za utafiti zaidi ya 20. Mandhari inayozunguka makao makuu inavutia sana. Maji ya ziwani ni maagavu yakionesha kivuli cha majengo, miti na mianzi inafungamana, mazingira ni shwari, kwa jumla ni mahali pazuri pa kufanyia utafiti kwa makini. Wanaotaka kujiunga na timu yetu wanakaribishwa.

Auani: Kitivo cha Utafiti wa Afrika, Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang, nambari 688, Mtaa

wa Yingbin, mji wa Jinhua, Mkoa wa Zhejiang, China

Nambari ya posta: 321004

Nambari ya simu: +86 579 82286091

Kipepesi: +86 579 82286091

Barua pepe: ias@zjnu.cn